Makala hii imeendelea kutoka Sehemu ya 1 ambapo tulizungumzia 'Lishe'.
MAZOEZI Kwa kawaida, katika sehemu hizi mbili yaani lishe na mazoezi, hii ya mazoezi ndio sehemu rahisi zaidi.
Ikiwa wewe ni mnene, kuna uwezekano haufanyi mazoezi. Labda hujafanya mazoezi kwa muda mrefu sana. Usiwe na wasiwasi, muda umeshapita lakini unaweza kujaribu kuboresha leo yako na kesho yako kwa kuanza mazoezi.
Mazoezi kama tunavyofahamu yana faida nyingi kama vile kuimarisha afya, kuboresha hali ya mhemko, kukuza afya kwa jumla na kinga, nk. (tayari unajua hili)
Nipo hapa kukupa ushauri wa vitendo ili kukusaidia uanze na kudumisha safari yako ya kupunguza uzito.
Kwa kuanzia, tutafanya zoezi moja kwa siku ndani ya mwezi wa kwanza - hapa kuna mazoezi rahisi ambayo unaweza kufanya asubuhi;
Kukimbia dakika 30 (dakika 1 kukimbia - dakika 1 kutembea - badilisha mara 15)
Kujinyoosha mwili mzima
Squats 60
Push-ups 60
Sit-ups 60
Ongeza idadi hapo juu hadi 100 kwa kila mojawapo (squats/push-ups/sit-ups) kwa mwezi kama unajisikia uko tayari kufanya hivyo.
Ikiwa uko mnene sana, push-ups na squats sio rahisi kwa sababu ya madhara yanayoweza kutokea kwenye viwiko na magoti yako. Ningependekeza kuendelea na zoezi la kukimbia kwa dakika 30 kwa mazoezi ya asubuhi mpaka uzito wako utakapokuwa wa kawaida zaidi.
Baada ya mwezi mmoja, tutaanza na mazoezi ya jioni (pamoja na mazoezi ya asubuhi), ambayo yatakuwa mazoezi ya KUIMARISHA MISULI.
Mazoezi ya kuimarisha misuli ni muhimu sana kwa afya. Huchangia misuli na kukufanya uwe imara na kuondoa mafuta (uzito) na udhaifu.
Utahitaji kujiunga na gym iliyo karinu nawe. Ikiwa unaishi mjini, utapata machaguo mengi zaidi ya bei nafuu karibu nawe.
Unapaswa pia kuajiri mwalimu binafsi (personal trainer) ikiwa unaweza kumudu. Mwalimu binafsi anaweza kukurahisishia safari yako ya kuboresha afya yako na azma yako ya kwenda gym.
Ikiwa huwezi kumudu kuajiri mwalimu binafsi, kuna rasilimali nyingi mtandaoni unazoweza kutumia kujifunza.
Kuna watu ambao wapo mitandaoni hasa instagram na wanatoa huduma hizo, mmojawapo ni Denzel Trainer kwa mwongozo zaidi juu ya mazoezi ya kuimarisha misuli pamoja na afya kiujumla, ikiwa huna uzoefu au mwalimu na huwezi kumudu basi angalia vitabu kama Burn the Fat, Feed the Muscle (Kitabu Kizuri Sana!).
Unaweza kupata programu nyingi za mazoezi mtandaoni, google search inaweza kusaidia. Au unaweza kuunda mpango wako wa mazoezi mwenyewe na ukakusaidia sana.
Pia unaweza kupata mazoezi yanayofaa kufanyia nyumbani ikiwa huwezi kumudu uanachama wa gym.
Mambo zaidi:
Mazoezi ya asubuhi lazima yafanyike KILA SIKU. Hakuna njia nyingine. Aidha, itakusaidia kuamka na kubaki macho wakati wote wa siku. Udai mwili wako na ujitume, hakika itakulipa.
Mazoezi ya kuimarisha misuli ni mara 4 kwa wiki labda kama mwalimu wako anapendekeza ratiba nyingine.
Kumbuka, mazoezi ya kuimarisha misuli ni msingi wa misuli na uhai. Itakusaidia kuchoma mafuta zaidi hata ukiwa umepumzika kutokana na athari yake ya kuchoma mafuta baada ya kumaliza mazoezi.
Namna ya kudili na maumivu ya misuli.
Oga kwa maji ya baridi na moto kwa pamoja. Ni rahisi, badilisha kati ya maji ya moto na baridi. Maji ya moto hufanya mishipa ya damu kufunguka na kuongeza mtiririko wa damu. Maji baridi hufanya mishipa ya damu kusinyaa na kupunguza mtiririko wa damu. Inasaidia kupona maumivu ya misuli na pia kuchoma kalori. Napendekeza kufanya hivyo mara moja baada ya mazoezi.
Makala hii imeendelea katika Sehemu ya 3: Mazoezi kama mtindo wa maisha.
0 Maoni